Searching for Methali za Kiswahili. Today we are going to look at Methali za Kiswahili. You can use them in your saying or writing Isha.
A
- Ada ya mja hunena, mwungwana ni kitendo.
- Adhabu ya kaburi aijua maiti
- Afua ni mbili, kufa na kupona.
- Ahadi ni deni.
- Aibu ya maiti, aijua mwosha.
- Ajali haina kinga wala kufara
- Aisifuye mvua, imemnyeshea.
- Akiba haiozi.
- Ajidhaniye amesimama, aangalie asianguke.
- Asifuye mvuwa imemnyea.
- Akili nyingi huondowa maarifa.
- Akili ni nywele; kila mtu ana zake.
- Akitaka kaa, mpe moto.
Read: Kiswahili Insha Examples
- Akipenda chongo huita, huona kengeza.
- Akufukuzaye hakwambii, Toka.
- Akupaye kisogo si mwenzio.
- Akumulikaye mchana; usiku akuchoma.
- Aliyekando, haangukiwi na mti.
- Alalaye usimwamshe; ukimwamsha, utalala wewe.
- Aliyeko juu, mungojee chini.
- Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga.
- Amnyimae punda adesi, kampunguzia mashuzi.
- Asiye kuwapo na lake halipo.
- Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu
- Asiyekuwapo na lake halipo.
- Asiyekujua hakuthamini.
- Asiye kubali kushindwa si mshindani.
- Asiyesikia la mkuu, huvunja guu
- Atangaye na jua hujuwa.
- Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
- Avuaye nguo huchutama.
B
- Baada ya kisa mkasa. Baada ya chanzo kitendo.
- Baniani mbaya kiatu chake dawa.
- Baada ya dhiki faraja.
- Bendera hufuata upepo.
- Baniani mbaya kiatu chake dawa.
- Bora afya kuliko mali.
- Bilisi wa mtu ni mtu.
Read: KCPE Kiswahili Revision Paper With Answers
C
- Chanda chema huvikwa pete.
- Chamlevi huliwa na mgema.
- Cha kuvunda, hakina ubani.
- Chema chajiuza, kibaya chajitembeza
- Chombo cha kuzama hakina usukani.
- Chembe na chembe ni mkate.
- Cha kichwa kitamu, na cha mkia kitamu.
- Chovya chovya yamaliza buyu la asali.
- Cha kuvunja, hakina rubani.
- Chema hakikai
- Chombo kilichopikiwa samaki hakiachi kunuka vumba.
- Chui hageuki madoamadoa
- Chungu kikuu, hakikosi ukoko.
Read: African Proverbs
D
- Dalili ya mvua mawingu.
- Dau la mnyonge haliendi joshi; likienda joshi ni mungu kupenda.
- Damu nzito kuliko maji.
- Debe shinda haliachi kutika.
- Dawa ya moto ni moto.
- Dunia duwara.
- Dua la kuku halimpati mwewe.
- Duniani ni msiba na furaha, kuna ugonjwa na siha.
- Dunia huleta jema na ovu.
- E
- Elimu bahari, haina kuta wala dari.
- F
- Fadhila ya punda ni mateke.
- Faragha ya nyani, huishia ngokoni
- Fimbo ya mbali hayiuwi nyoka.
- Fahali wawili hawakai zizi moja.
- Fuata nyuki ule asali.
- Fedha fedheha.
- Fumbo mfumbe mjinga mwerevu huligangua.
- Fungato haliumizi kuni.
Read: Debate Motions for Secondary Schools in Kenya
G
- Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.
H
- Haba na haba hujaza kibaba.
- Habari ya uwongo, ncha zake saba, habari ya kweli, ncha yake moja.
- Hapana marefu yasio na mwisho.
- Hakuna bahari, isiyo na mawimbi.
- Hakuna siri ya watu wawili.
- Haraka haraka haina baraka.
- Hasira, hasara.
- Hasira za mkizi, tijara ya mvuvi
- Hakuna kisicho badali.
- Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
- Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
- Hiari ya shinda utumwa.
- Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
- Hapana marefu yasio na mwisho.
- Heri kuliwa na simba, kuliko kuliwa na fisi.
- Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
J
- Jina jema hungara gizani.
- Jitihadi haiondoi kudura ya mungu.
- Jogoo la shamba haliwiki mjini.
- Jino la pembe si dawa ya pengo.
- Jivu halijai, gao la mkono.
Read: CBC Curriculum Structure
K
- Kamba hukatika pabovu.
- Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
- Kama chanda na pete.
- Kanga hazai ugenini.
- Kata pua uunge wajihi
- Kawia ufike
- Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
- Kelele za mlango haziniwasi usingizi.
- Kenda karibu na kumi.
- Kidole kimoja hakivunji chawa.
- Kidogo ni tamu, kingi ni sumu.
- Kichache hakikutoshi na kingi hakikulishi.
- Kiburi si maungwana.
- Kikulacho ki nguoni mwako.
- Kila mlango na ufunguo wake.
- Kila chombo kwa wimbile.
- Kingiacho mjini si haramu.
- Kila ndege huruka na mbawa zake.
- Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
- Kinyozi hajinyoi, akinyoa kujikata.
- Kipendacho moyo ni dawa.
- Kipofu haonyi njia.
- Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
- Kila ndege mwenye mkia ni lazima aringe.
- Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
- Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
- Kinolewacho, hukata.
- Kilichomo baharini, kakingojee ufukoni.
- Kiozacho hutoa uvundo
- Kipofu hasahau fimbo yake
- Kinywa ni jumba la maneno.
- Kipya kinyemi ingawa kidonda.
- Kisokula mlimwengu,sera nale.
- Kitanda usicho kilala hujui kunguni wake.
- Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
- Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
- Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwengu uwishe.
- Kobe atakufa asipojikuna nyumaye mwenyewe.
- Kosa moja haliachi mke.
- Konzo ya maji haifumbatiki
- Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
- Kufa kikondoo, ndiko kufa kiungwana.
- Kufa kufaana.
- Kuchamba kwingi,kuondoka na mavi.
- Kuku havunji yai lake.
- Kukopa harusi, kulipa matanga.
- Kufa kwa mdomo, mate hutawanyika.
Read: 100 Positive Behavior Quotes for Students
- Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
- Kuku wa maskini hatagi mayai.
- Kuku mwenye watoto, halengwi jiwe.
- Kucha M’ngu si kilemba cheupe.
- Kufa si suna,ni faradhi.
- Kujikwa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
- Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana.
- Kuagiza kufyekeza.
- Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
- Kunako matanga kumekufa mtu.
- Kumpa mwenzio si kutupa, ni akiba ya mbeleni.
- Kupanda mchongoma ,kushuka ngoma.own.
- Kupotea njia ndiyo kujua njia.
- Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
- Kusikia si kuona.
- Kuuliza si ujinga.
- Kutu kuu ni la mgeni.
- Kwenye miti hakuna wajenzi.
- Kwenda mbio siyo kufika.
- Kweli iliyo uchungu si uwongo ulio mtamu.
L
- La kuvunda (kuvunja)halina ubani.
- Lake mtu halimtapishi bali humchefusha.
- La kuvunda halina rubani.
- Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
- Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
- Leo uko, kesho huko.
- Liandikwalo ndiyo liwalo.
- Likitoka liote.
- Lipitalo ,hupishwa .
- Lifaalo kueleza lieleze, lisilofaa limeze.
- Lila na fila hazitangamani.
- Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
- Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
Read: Best Quotes about Education
M
-
- Macho hayana pazia.
- Maafuu hapatilizwi.
- Mafahali wawili hawakai zizi moja.
- Maisha hayana pato, hutupita kama ndoto.
- Mahaba haiwi mlango.
- Maiti haulizwi sanda.
- Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaogelea.
- Maji hufuata mkondo.
- Maji huteremka bondeni, hayapandi mlima.
- Maji yakija hupwa.
- Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
- Maji yakimwagika hayazoleki
- Maji ya nazi, yataka uvugulio tu.
- Maji yakija hupwa.
- Maji yaenda njia yake.
- Maji ya kifuu ni bahari ya chungu.
- Maji ya moto, hayachomi nyumba.
- Majumba makubwa husitiri mambo.
- Mpanda ngazi hushuka.
- Majuto ni mjukuu.
- Mali ya bahili huliwa na wadudu.
- Mambo ya mbele, giza ya wele
- Mambo ya nyumba, ni kinga.
- Manahodha wengi chombo huenda mrama.
- Maneno mema hutowa nyoka pangoni.
- Maneno makali hayavunji mfupa.
- Maneno mengi si haja, maneno mengi si huja.
- Masikini akipata matako hulia mbwata.
- Maskini haokoti, akiokota huambiwa kaiba.
- Maskini na mwanawe, tajiri na mali yake.
- Masikio hayapiti kichwa.
- Mapema maivu, mapema maovu.
- Mapaka wengi, hayamkamati panya.
- Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
- Mapenzi ni majani, popote penye mbolea huotea.
- Mara changu, mara chako
- Mavi usioyala,wayawingiani kuku?
- Mavi ya kale hayanuki.
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
- Mbinu hufuata mwendo.
- Mbiu ya mgambo ikilia ina jambo.
- Mbuzi wa maskini, hazai mapacha
- Mbwa hafi maji, akiona ufuko.
- Mbinu hufuata mwendo.
- Mbuge hawezi kujenga nyumba.
- Mbuzi wa mkata, atakufa utasa.
- Mchagua jembe si mkulima.
- Mcheka kilema, hafi bila kumfika.
- Mchelea mwana kulia hulia yeye.
- Mchelea bahari si msafiri.
- Mchagua nazi, hupata koroma.
- Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
- Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
- Mchana semani usiku lalani.
- Mchele moja mapishi mengi.
- Mcheka kilema hafi bila kumpata.
- Mcheza kwao hutuzwa.
- Mchimba kisima huingia mwenyewe.
- Mcheza na tope humrukia.
- Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
- Mchezea zuri, baya humfika.
- Mchimba kisima, hakatazwi maji.
- Mchovya asali hachovi mara moja.
- Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
- Mchuma janga hula na wakwao.
- Mchumia juani,hula kivulini.
- Mchuma janga hula na wakwao.
- Mchunga haziki.
- Mdharau biu hubiuka yeye.
- Mema na mabaya ndio ulimwengu.
- Meno ya mbwa hayaumani.
- Mficha uchi hazai.
- Mfa maji hukamata maji.
- Mfinyazi hulia gaeni.
- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
- Mganga hajigangui.
- Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
- Mgeni ni kuku mweupe.
- Mgonjwa haulizwi uji.
- Mgeni njoo mwenyeji apone.
- Mgonjwa haulizwi uji.
- Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
- Milima ya mbali, haina mawe
- Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
- Mjumbe hauawi.
- Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
- Mkeka mpya haulaliwi vema.
- Mkamia maji hayanywi.
- Mkono moja haulei mwana.
- Mkono moja hauchinji ngombe.
- Mkono mtupu haulambwi.
- Mkono usioweza kuukata, ubusu.
- Mkosa jembe halimi
- Mkono wa kuume, haukati wa kushoto.
- Mkosa kitoweo humangiria.
- Mke ni nguo ,mgomba kupalilia.
- Mkosa titi la mama, hata la mbwa hulamwa.
- Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
- Mkuki kwa nguruwe mtamu,kwa mwanadamu uchungu.
- Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
- Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekeya.
- Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
- Mla mla leo mla jana kala nini?
- Mla mbuzi hulipa ngombe.
- Mla cha uchungu na tamu hakosi.
- Mla kwa miwili, hana mwisho mwema.
- Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
- Mlevi wa mvinyo hulevuka, mlevi wa mali halevuki.
- Mlimbua nchi ni mwananchi.
- Mlinzi hulinda ndege, mke mzuri halindwi.
- Mnyonge hana hasira.
- Moja shika,si kumi nenda urudi.
- Mmoja hashui chombo.
- Mnyamaa kadumbu.
- Mnywa maji kwa mkono moja,Kiu yake i pale pale.
- Mnyonyore haunuki, hupendeza maua yake.
- Mnyonge hupata haki, ni mwenye nguvu kupenda.
- Moto hauzai moto.
- Moja shika, kumi hutapata
- Moja shika si kumi nenda urudi.
- Moto wa kumvi,hudumu.
- Mpanda ngazi hushuka.
- Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
- Mpemba akipata gogo hanyii chini.
- Mpanda ovyo hula ovyo.
- Mpemba hakimbii mvua ndogo.
- Mpende akupendaye.
- Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia
- Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
- Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
- Msema kweli, hana wajoli.
- Mshoni hachagui nguo.
- Mshale usiyo na nyoya, hauendi mbali.
- Msasi haogopi mwiba.
- Mshale kwenda msituni haukupotea.
- Msema pweke hakosi.
- Mshika mawili, moja humponyoka.
- Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
- Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
- Msika mavi, hayaachi kumnuka.
- Msi chake ni mwenda zake.
- Mstahimilivu hula mbivu.
- Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
- Mtaka yote hukosa yote.
- Mtafunwa na nyoka akiona ung’ongo husitika.
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
- Mtaka unda haneni.
- Mtegemea nundu haachi kunona.
- Mtaka yote kwa pupa, hukosa yote.
- Mtembezi hula miguu yake.
- Mteuzi hashi tamaa.
- Mtego bila ya chambo, haunasi.
- Mtenda mema hasemi, akisema hatendi.
- Mti hauendi ila kwa nyenzo.
- Mti huponzwa na tundaze.
- Mti upigwao mawe ni mti wenye matunda.
- Mtoto akililia wembe mpe.
- Mtoto wa nyoka ni nyoka.
- Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
- Mtondoo haufi maji.
- Mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha mamaye.
- Mtu hujikuna ajipatiapo.
- Mtumi wa kunga haambiwi maana.
- Mtu akimpa maskini kichache, Mungu humruzuku kingi.
- Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
- Mtu aliyeumwa na nyoka akiona ung’ongo hushtuka.
- Mtu apandacho (kitu), ndicho avunacho.
- Mtu pweke, ni uvundo.
- Mtu asiye na akili, usifuatane naye.
- Mtu huenda na uchao, haendi na utwao.
- Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
- Mtu halindi bahari, ipitayo kila chombo.
- Mtu hasafiri nyota ya mwenziwe.
- Mtu huulizwa amevaani haulizwi amekulani.
- Mtumi wa kunga haambiwi maana.
- Mtumikie kafiri upate mradi wako.
- Mtumai cha ndugu hufa masikini.
- Mume wa mama ni baba.
- Mtunza bahari, siye msafiri.
- Mtumikie kafiri upate mradi wako.
- Mtulivu hula mbivu.
- Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
- Mume ni kazi, mke ni nguo.
- Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendo wake.
- Mume wa mama ni baba.
- Mungu hapi kwa mvua, wala hanyimi kwa jua.
- Muhogo mchungu, usiuchezee.
- Mungu hamfichi mnafiki.
- Muuliza hujibiwa ili apate fahamu.
- Mvuvi ajuwa pweza alipo.
- Mvumbika changa hula mbovu.
- Mvunja nchi ni mwananchi.
- Mvungu mkeka.
- Mvuvi ajuwa pweza alipo.
- Mwamini Mungu si mtovu.
- Mwana kila mwaka, ni kubwa baraka.
- Mwacha asili ni mtumwa.
- Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
- Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
- Mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idi.
- Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
- Mwanadamu atakufa, jina lake litakaa.
- Mwanamaji, hutaraji kufa maji.
- Mwanamume ni mbono, hualikia kule.
- Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
- Mwanga mpe mtoto kulea.
- Mwana simba ni simba.
- Mwanzo kokochi mwisho nazi.
- Mwana wa mtu ni kizushi; akizuka, zuka naye.
- Mwangaza mbili moja humponyoka.
- Mwanzo wa ngoma ni lele.
- Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
- Mwenda bure si mkaa bure huenda akaokota.
- Mwenda mbio hujikwa kidole.
- Mwenye kelele hana neno.
- Mwenye huba, hana dawa, ila kwa muhibiwa.
- Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
- Mwapiza la nje hupata la ndani.
- Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
- Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
- Mwenye chake, hakosi cha mwenziwe
- Mwenye nguvu mpishe.
- Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
- Mwenye kovu, usidhani kapoa.
- Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
- Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
- Mwenye kutafuta, hakosi kupata.
- Mwenye shoka hakosi kuni.
- Mwenye kovu, haliwai na kidonda.
- Mwenye kovu usidhani kapowa.
- Mwenye kupenda ni juha.
- Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
- Mwenye kisu kikali ndiye alaye nyama.
- Mwenye kupanda ngazi, na mwenye kushuka ngazi, hawapeani mkono.
- Mwenye macho, haambiwi tazama.
- Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
- Mwenye njaa hana miiko.
- Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
- Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
- Mwenzako akinyolewa wewe tia maji
- Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
- Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
- Mwiba wa kujitoma, hauambiwi pole.
- Mwizi, siku zake ni arobaini
- Mwosha hadhuru maiti.
- Mwosha husitiri maiti.
- Mwomba chumvi huombea chunguche.
- Mzazi haachi ujusi.
- Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
- Mzoea punda, hapandi farasi.
- Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
- Mzika pembe ndiye mzua pembe.
- Mzoea udalali, duka haliwezi.
- Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
N
- Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
- Nazi mbovu harabu ya nzima.
- Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu
- Ncha na ncha, hazichomani
- Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
- Ndugu chungu, jirani mkungu.
- Ndege mwigo hana mazowea.
- Na tuone ndipo twambie, kusikia si kuona.
- Ndege hulindwa, mke halindwi.
- Ndimi arobaini, mafundo arobaini.
- Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
- Ndovu halemewi na pembe zake.
- Neno ulikataalo, ndilo Mungu apendalo.
- Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
- Ngoma ivumayo haidumu.
- Ngozi ivute ili maji.
- Ng’ombe haelemewi na nunduye.
- Ng’ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
- Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
- Nguruwe aendealo, ndilo atendalo.
- Nguo za kuazima, hazisitiri matako.
- Nifae na mvua nikufae na jua.
- Ni heri mbichi, kama ya kwoka.
- Ni jambo lipi, lisilo na nduguye, na mwamu wake.
- Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
- Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
- Njia ya mwongo fupi.
- Njaa ya leo, ni shibe ya kesho.
- Njema haziozi.
- Njia ya siku zote haina alama.
- Nyota haionekani mchana.
- Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
- Nta si asali nalikuwa nazo si uchunga.
- Nyoka, mlinzi wa pango lake.
- Nyumba haikimbii.
- Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
- Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu.
- Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
- Njia mbili zilimshinda mzee fisi, alipasuka msamba.
P
- Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
- Paka akiondoka, panya hutawala.
- Pabaya pako si pema pa mwenzako.
- Painamapo ndipo painukapo.
- Paka wa nyumba haingwa.
- Paka hakubali kulala chali.
- Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
- Panapo wengi hapaharibiki neno.
- Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
- Penye kuku wengi hapamwagwi mtama.
- Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
- Penye dhiki, hakuna chuki.
- Penye miti hakuna wajenzi.
- Penye urembo ndipo penye urimbo.
- Penye nia ipo njia.
- Penye wazee haliharibiki neno.
- Penye wengi pana mengi.
- Penye wengi pana Mungu.
- Pesa na zawadi hufanya miadi.
- Pilipili usozila zakuwashiani?
- Pwagu hupata pwaguzi.
- Punda haendi ila kwa kigongo.
- Punge moja ya mtama, ni bora kuliko almasi.
- Pofu hasahau mkongoja wake.
R
- Radhi ni bora kuliko mali
S
- Samaki mmoja akioza, huoza wote.
- Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
- Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
- Shika! Shika! na mwenyewe nyuma.
- Samaki huanza kuoza kichwani.
- Shibe ya mtu mwingine hanilazi mnene.
- Saburi ni ufunguo wa faraja.
- Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
- Shimo la ulimi mkono haufutiki.
- Sikio la kufa halisikii dawa.
- Sikio halilali na njaa.
- Sikio halipwani kichwa/Sikio halipiti kichwa.
- Sikio halipwani kichwa.
- Siku njema huonekana asubuhi.
- Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama.
- Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
- Subira ni ufunguo Wa faraja.
- Subira yavuta heri, huleta kilicho mbali.
- Sumu ya neno ni neno.
- Suluhu haija ila kwa ncha ya upanga.
- Sitafuga ndwele na waganga tele.
- Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
T
- Tamaa mbele, mauti nyuma.
- Teke Ia kuku halimwumizi mwanawe
- Tamu tulikula sote, na uchungu vumilia.
- Tonga si tuwi
- Taratibu ndiyo mwendo.
- Tabia ni ngozi.
- Tajiri na maliye,maskini na mwanawe.
- Taratibu ndiyo mwendo.
- Titi la mama li tamu.
U
- Udongo uwahi ungali maji
- Ukenda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
- Uchungu wa mwana, aujua mzazi.
- Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
- Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
- Ubishi mwingi, huvuta matata
- Udugu wa nazi hukutania chunguni
- Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
- Uchwelewapo na jua lala pale.
- Ujinga wa kuuza si baradhuli wa kununua.
- Ukiona vinaelea, vimeundwa.
- Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
- Ukitaka uzuri sharti udhurike.
- Ukamba hukatika pabovu.
- Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
- Ulimi hauna mfupa.
- Ukikosa titi la mama, hata la mbwa huamwa
- Ukiona zinduna, ambari iko nyuma.
- Ukila na kipofu sahani moja, usimguse vyanda.
- Ukienda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
- Ukipewa shibiri usichukue pima.
- Ukupigao ndio ukufunzao.
- Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Fir-Auni.
- Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
- Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
- Ukitaka cha mvunguni, sharti uiname.
- Ukitaka uzuri sharti udhurike.
- Ulacho ndicho chako, kilichobaki nicha mchimba lindi.
- Ulipendalo hupati hupata ujaliwalo.
- Ulimi unauma kuliko meno.
- Ulivyoligema utalinywa.
- Umekuwa bata akili kwa watoto?
- Umekuwa jeta hubanduki?
- Umwepuke, mwenda-pweke.
- Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
- Usiache kunanua kwa kutega.
- Upikapo samaki, huachi kunuka vumba.
- Uniponye kwa jua, nitakuponya kwa mvua.
- Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
- Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
- Ushikwapo shikamana.
- Usiache mbachao kwa msala upitao.
- Usigombe na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
- Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
- Usitukane wakunga na uzazi ‘ungalipo.
- Usijifanye kuku mweupe.
- Usile na kipofu ukamgusa mkono.
- Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
- Usisafiriye na nyota ya mwenzio.
- Usimwamshe aliyelala utalala wewe.
- Usinivishe kilemba cha ukoka.
- Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
- Usidharau kiselema chalima kikapita jembe zima.
- Usipoziba ufa utajenga ukuta.
- Uta hauui bila upote
- Uzuri wa mke nguo, wa ng’ombe kulimwa.
- Uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha mti.
- Uzuri wa godoro wa nje tu, kwa ndani mna pamba
- Usiwashe taa, nyumbani mwa kipofu.
V
- Vita havina macho.
- Vita ya panzi, furaha ya kungu.
- Vikombe vikikaa pamoja, havina budi kugongana.
- Vita vya panga, haviamuliwi na fimbo.
W
- Waraka hauishi maneno.
- Watafutao, wapata.
- Wanao usawa gani, hakimu na baradhuli.
- Wakati wa hari, watu wagombea kisima kimoja.
- Wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi.
- Waraka ni nusu ya kuonana.
- Wema hauozi.
- Wengi wape.
- Werevu mwingi, mbele kiza
- Weka siri moyoni, kunena ni kutolea.
- Watatuavu, hutatua.
- Watu wawili hawashibi: mtaka elimu na mtaka ulimwengu.
Y
- Yu fahali nyati na mali hapati.
- Yaliyopita, yamepita, yaliyobaki, tuyatupe.
- Ya kunya, haina wingu.
- Yapitayo hayabadiliki, na yajayo hayaelimiki.
Z
- Zito huwa pesi (nyepesi) ukilichukua.
- Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Betty is a qualified teacher with a Bachelor of Education (Arts). In addition, she is a registered Certified Public Accountant. She has been teaching and offering part-time accounting services for the last 10 years. She is passionate about education, accounting, writing, and traveling.